Monday, December 22, 2008

RATIBA YA WIKI WRM

Siku ya Jumanne ni jinsi ya kuutunza uponyaji-saa10:00-12:00 jioni.
Siku ya Alhamisi ni jinsi ya kuukulia wokovu --saa10:00-12:00 jioni
Siku ya Jumamosi ni ibada ya maombezi -saa 9:00-12:00jioni
Siku ya Jumapili kuna ibada 2 za maombezi asubuhi na jioni saa 3:00 asubuhi -7:00 mchana.Na saa 10:00 -12:00 jioni. KARIBUNI WOTE,TUPO KITUNDA KIVULE-KITUO CHA BUSTANI YA EDENI ZAMANI MATEMBELE YA KWANZA YAKIVULE. KWA MAWASILIANO ZAIDI;0755 448116,0784 448117

Tuesday, December 16, 2008

MIUJIZA YAZIDI KULIPUKA WRM

Wakazi wa jiji la Dar es Salaam na nje ya jiji hilo wanaohudhuria katika huduma ya maombezi ya The Word of Reconciliation Ministries (WRM) lililochini ya Mchungaji Nicolaus Suguye wamezidi kupokea miujiza yao kutoka kwa Mungu baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa miaka mingi bila kupona.(Kulia Mchungaji Suguye akiingia katika Huduma ya The Word of Reconcilion Ministries)

Katika hali ya kushangaza watu wengi Eliza Mwita binti aliyezaliwa akiwa kipofu aliombewa katika huduma hiyo na kunza kuona kama kawaidi, huku bibi Sisilia Biti Gulasa ambaye hakuweza kuitambua miaka yake kutokana na uzee, aliponywa ugonjwa wa moyo uliokuwa unamsumbua kwa miaka mitano huku akimaliza kila aina ya tiba bila mafanikio.
Bibi huyo alisema usiku alikuwa halali kutokana na maumivi makali aliyokuwa akiyapata, na alipoenda hospitali kupima alibainika ana moyo alipewa dawa za kila aina lakini haikusaidia mpaka alipoamua kusalimisha maisha yake kwa Yesu ( kuokoka) ndipo alipokea mjiza wa uponyaji.
Alisema kabla ya uponyaji huo alitumia gharama kubwa ya kutaka kuokoa maisha yake kutokana na maumivu makali yaliyokuwa yanamsumbua na kupelekea asipate usingizi nyakati za usiku, lakini baada ya uponyaji huo maumivu hayo hayakumbuki tena na anapata usingizi
safi.
Mbali na hao watu wengine ambao Mungu aliamua kuwaponya na kujitukuza kupitia kwa Mtumishi wake Suguye ni Jastine Mahoka ambaye alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya mguu kwa muda mrefu na kupelekea ashindwe kutembea kutokana na mguu huo kuoza na kutoa harufu kali, alijikuta anatembea kama kawaida baada
ya kufanyiwa maombi katika huduma hiyo iliyopo Matembele ya Kwanza Kivule nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. (kushoto Mchungaji Suguye akimwombea Eliza aliyekuwa kipofu baada ya kufikishwa katika huduma ya Maombezi)
Naye baba mmoja aliyejulikana kwa jina moja, alijikuta anapona vidonda vya tumbo ambavyo vilikuwa vinamsumbua kila nyakati za usiku, na kutumia kila aina ya dawa bila mafanikio huku akipinga uweza wa Mungu
kama anaweza kupona ugonjwa huo.
Akisimuliwa mkasa huo kwa niaba ya mke wake, Maria Sande alisema kuwa mumewe kwa murefu alikuwa anakaidi kwenda katika makanisa ya Kiroho kutokana na kukumbatia dini yake, hata hivyo baada ya kuzidiwa na ugonjwa huo aliomba apelekwe katika huduma hiyo kwenda kuombea baada ya kusikia kuwa watu wengi wenye magonjwa yaliyoshindikana kibinadamu wanaponywa kwa uwezo wa Mungu.
Suguye alisema kuwa watu wengi wamekuwa wakibeza miujiza inayotendeka katika huduma zinazotolewa na watumishi waliopakwa mafuta na Mungu, na kujikuta wanakimbilia kwa waganga wa kienyeji hali ambayo huwasababishia kupoteza fedha nyingi kwa kuwapa waganga hao huku wakikimbia huduma inayotolewa bure na Mungu.
Katika hatua nyingine Mchungaji Suguye alisema kuwa huduma yake ya The Word of Reconciliation Ministries (WRM), inatarajia kufungua chuo cha watumishi wa Mungu kitakachojulikana kwa jina la The Reconciliatio Pastors & Prophets College.
Chuo hicho kinatarajiwa kuanza Januari 1 mwakani kikiwahusisha watu wote wenye wito na kazi ya Mungu watakaomtumikia bila kubagua dini ama dhehebu lolote kwa lengo la kuwa kulitangaza vema neno la Mungu kila pembe ya nchi na dunia kwa ujumla. Hata hivyo tayari nafasi hizo zimeshajaa kwa sasa na kwa watakaotaka kujiunga na chuo hicho waombe nafasi hiyo mwezi April 2009.


Ratiba
Jumamosi saa 9:00 mchana mpaka 12:00 jioni maombezi
Jumapili kuna ibaada mbili
1.Saa
2:00 asubuhi mpaka 7:00

2. Saa 10:00 – 12:00

Jinsi ya kufika katika huduma hiyo, panda magari mpaka Banana, kisha panda magari ya kwenda Kivule, shuka Bustani ya Edeni zamani Matembele ya kwanza Kivule kisha uliza Huduma ya Neno la Upatanisho (The Word of Reconciliation Ministries) watakuelekeza. Wote mnakaribishwa kwa ajili ya uponyaji na matatizo mbalimbali yaliyoshindikana. Ama piga simu no. 0784 448117 au 0715 448117.

TUSITOZE FEDHA KWA AJILI YA SEMINA ZA NDOA

Watumishi wa Mungu nchini wametakiwa kuacha kasumba ya kuwatoza fedha waumini wao kwa ajili ya kuwafundisha masomo ya ndoa ili kuziponya ndoa zao.

Kauli hiyo imetolewa na Mchungaji Nicolaus Suguye wa Huduma ya Maombezi ya The Word of Reconciliation Ministries lililopo Kivule Bustani ya Edeni zamani 'Matembele ya Kwanza' nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, aliyesema kuwa kufanya hivyo ni kushindwa kuwatendea haki wanandoa walio na kipato cha chini.Mchungaji Nicolaus Suguye wa Huduma ya maombezi, The Word of Reconciliation Ministries akifundisha somo la ndoa.
Mchungaji Suguye alisema kitendo cha kuwatofa fedha wanandoa hao kunasababisha wanandoa wengi hasa wenye kipato cha chini kushindwa kuhudhuria katika semina hizo, nakujikuta wakiendelea kuishi maisha ya shida katika ndoa zao.
“ Si jambo la busara kuwatoza fedha wanandoa kwa ajili ya kuendesha semina za somo hilo, k
wa sababu kufanya hivyo kunasababisha somo hilo muhimu walipate watu wenye uwezo kifedha pekee na kujikuta wasiokuwa na pesa wanashindwa kuhudhuria katika semina hiyo kutokana na kipato chao kutoruhusu na hali hiyo imekuwa ikiendelea kuwafanya familia zisizo na fedha kuendelea kuishi maisha ya shida,” alisema Suguye. (Chini Mama Mchungaji akiimba wimbo wa kuabudu baada ya somo la semina ya ndoa)
Katika hatua nyingine Mchungaji Suguye aliwataka watumishi hao kuwa na utaratibu wa kuwafundisha somo la ndoa waumini wao ili kujenga kanisa lililotakatifu kuliko ilivyo kwa maadhi ya makanisa ambayo yamepoa kiroho kutokana na familia nyingi kuwa katika migogoro ya ndoa.
Alisema kanisa lilikiwa na familia ambazo ndoa zake hazina matatizo, Roho wa Mungu hushuka katika ibada na kuhudumia watu wenye shida ikiwa ni pamoja na kuwaponya wenye magonjwa yaliyoshindikana, kwa sababu kila aliyeingia ndani ya kanisa
hilo moyo wake unakuwa na furaha toka nyumbani kwake.
Aidha Mchungaji Suguye alisema siku zote ibada huanzia nyumbani, ambapo wanandoa wanapotoka nyumbani kwao wakiwa wenye furaha, hata kanisani furaha hiyo huongezeka na kujikuta wanamwabudu Mungu katika Roho na kweli na kuifanya ibada hiyo iwe moto.
Alisema familia ikiwa na ndoa yenye amani, chemchem ya mafanikio huonekana hali ambayo husababisha kanisa kukua kiuchumi kutokana na waumini wake kuwa na uwezo kimaisha na kuwa wepesi katika suala la utoaji wa sadaka na fungu la kumi.

WATOTO YATAIMA WAPEWA ZAWADI


Watoto yatima wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupewa zawadi ya Sukari, sabuni za kufulia, na kuogea, nguo mbalimbali, mafuta ya kupaka pamoja na mchele.

HUDUMA YA KUWASAIDIA WAJANE NA WATOTO YATIMA TAFANYIKA WRM


Mchugaji Nicolaus Suguye akimpa zawadi mtoto yatima. Hivi karibuni mchungaji huyo alifanya huduma ya kuwapa zawadi watoto yatima na wanajane.

Monday, December 15, 2008

WAUMINI WAKIFUATILIA NENO LA MUNGU KWA MAKINI.

Hawa ni baadhi ya watu waliohudhuria huduma ya Maombezi ya The Word of Reconciliation Ministries wakimsikiliza mchungaji Nicolaus Suguye ambaye ni mwanzilishi wa huduma hiyo.

Monday, December 1, 2008

MCHUNGAJI NICOLAUS SUGUYE AKIMWAMBIA BINTI KUWA YESU ANAWEZA KUMPONYA UPOFU ALIKOKUWA NAO


Mchungaji Nicolaus Suguye akiwaonyesha waumini wa kanisa lake jinsi binti alivyo kipofu, na ataona baada ya maombezi kwa sababu Mungu bado anatenda kazi mpaka sasa. Binti huyo alizaliwa akiwa kipofu.